SUA yawanoa wabunifu wa mavazi kuinua uchumi wa viwanda vidogo

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimeendelea na jitihada zake za kuunga mkono  sera za nchi na mwelekeo wa taifa kuelekea kukuza uchumi wa viwanda kwa kuhakikisha  kinatoa wataalam wenye ujuzi na maarifa  ambayo yatasaidia katika  kuinua uchumi wa viwanda vidogo na vya kati ambavyo vimeanzishwa nchini.

SUA

Prof. Japhet Kashaigili

Hayo yamebainishwa na Prof. Japhet Kashaigili ambaye ni Mratibu wa Utafiti na Machapisho SUA wakati akifungua mafunzo ya kongano la nguo mjini Morogoro yaliyo ratibiwa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kupitia kitengo cha Sayansi ya Mlaji yaliyo wajumuisha mafundi nguo na wabunifu wa mavazi kwa mkoa wa Morogoro.

"Kituo cha Ubunifu Kilichoko  katika Kurugenzi hii kimejikita katika kutoa elimu ya bunifu  mbalimbali, hati miliki, tafiti, uhaulishaji wa Teknolojia kwa wanafunzi, watafiti na   wajasiriamali wa viwanda  vidogo na vya kati na Dhumuni kubwa la kituo hiki ni kutoa maarifa shirikisha , kuchochea ubunifu kwa kuunganisha  watu wenye fikra na mtizamo sawa  ndani na nje ya Chuo cha Sokoine cha Kilimo, lakini Kwa ujumla kituo hiki kinalenga kujenga bunifu na ujasiriamali kwa kuboresha mahusiano kati ya chuo, viwanda na taasisi nyingine za nje" Alifafanua Prof.Kashaigili

Prof.Kashaigili ameongeza sambamba na kitengo cha bunifu kilichoko  katika kurugenzi,  kitengo cha Sayansi ya Familia na Walaji  kilichoko Ndaki ya Kilimo,  kinalenga kuboresha bunifu, ujuzi, maarifa, tafiti zinazosaidia watu kufanya maamuzi yanayolenga ustawi, mahusiano,  na rasilimali ili kuweza kufikia maisha bora zaidi. 

Aidha Kashaigili amesema kitengo cha Sayansi ya Familia na Walaji   kinajikita katika maeneo mengi ikiwa ni pamoja na ubunifu na ushonaji mavazi, mpangilio na upambaji wa ndani ya nyumba pamoja na masuala yanayohusisha sayansi ya walaji.

"Mafanikio ya viwanda hivi ikiwemo viwanda vya Kongano la nguo Morogoro (KONGUMO) yanategemea namna viwanda hivi vinavyoweza  kuboresha teknolojia na kujenga uwezo na hatimaye kuzalisha aina nyingi zaidi za bidhaa za kuuza ndani na nje ya nchi hivyo kuongeza tija na faida kwa kutumia kiasi kidogo cha mtaji" Alifafanua Prof.Kashaigili

Mary Marcel, Mhadhiri na Mbobezi wa masuala ya ubunifu wa mavazi,Utengenezaji wa samani na mapambo ya ndani kutoka SUA

Kwa upande wake, Mary Marcel ambaye ni Mhadhiri na Mbobezi wa masuala ya ubunifu wa mavazi,Utengenezaji wa samani na mapambo ya ndani kutoka SUA amesema kutokana na mchango mkubwa unaotolewa na mafundi nguo hapa nchini katika utengenezaji wa mavazi Chuo kupita washirika wake  kimeona kuna haja ya kuwaongezaea ujuzi katika kazi yao ya ubunifu wa mavazi ili iweze kuwa na thamani zaidi.

"Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo zamani kilikuwa kinajulikana kinahusika na kilimo tu lakini hivi karibuni kuanzia mwaka 2010 Chuo kiliweza kujipambanua na kwenda kwenye Nyanja nyingine ambazo zinamuhusu zaidi mlaji, sasa kupitia kitendo cha cha sayansi ya mlaji wakajiweka zaidi kwenye ubunifu wa mavazi tukitambua mavazi ni kitu muhimu kwa binadamu na tukasema isiwe tu bora mavazi lakini lazima vazi liwe la ubunifu ili mtu anavyo vaa vazi na   muonekano wake uwendane, kwaiyo kupitia kitengo hichi cha ubunifu tukatambua kuwa kuna mafundi ambao wanasaidia kushona haya mavazi ndomaana leo tunawapa mafunzo" Alisema Mary Marcel

Naye Robert Joseph, Mwenyekiti wa KONGUMO la nguo Manispaa ya Morogoro akizungumza kwa niaba ya washiriki wengine amesema matarajio yao baada ya mafunzo ni kukakikisha wanafanya ubunifu wa mavazi  wenye tija na wenye kulenga soko la ndani nanje ya nchi huku akiongeza kuwa mafunzo hayo yatawabadilisha mafundi  katika kutekeleza kazi zao na kuongeza uaminifu kwa wateja

Robert Joseph Mwenyekiti wa  KONGUMO la nguo Manispaa ya Morogoro

 

Share this page